Thursday, 13 March 2014

HUYU MZEE NUSURU AFE KWA KUPAGAWA BAADA YA KULIPWA MILIONI SABIN HEBU SOMA HAPANa Mwandishi wa Xdeejayz- Bagamoyo
Kweli Mungu si Athumani au Ramadhani waswahili walisema hivyo.. Mzee mmoja mkazi wa Bagamoyo Mapinga hivi karibuni nusra apoteze maisha baada ya kukamata pesa taslimu zaidi ya milini 70 papo hapo kisha kupandisha Presure hadi kukimbizwa Hospitali.
Kwa mujibu wa mwandishi wetu wa Xdeejayz toka Bagamoyo alisema mzee huyo aliyefahamika kwa jina Mwinyimkuu Ramadhani "68" alipata pesa hizo baada ya kuuza shamba lake kwa mdosi mmoja ambae alimpa opusheni mbili kama anahitaji kupewa pesa keshi ama aingiziwe benki, lakini mzee huyo alikataa kusikia habari za kuwekewa pesa benki kwa kuhofia kudhurumiwa hivyo hivyo aletewe chake mkononi.
Ndipo mdosi huyo alipochukua mfuko wa pesa huo uliokuwa umefungwa milioni moja moja na kumkabidhi chake mzee huyo.
CREDIT:X-DEEJAYZ

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search