Thursday, 30 June 2016

BEN PAUL KUJA KIVINGINE BAADA YA RAMADHANI SASA KUFANYA TOUR NCHI NZIMA

June 30/06/2016 at 9:56 am


Ben Pol anajipanga kufanya ziara ya ‘Moyo Mashine Tour’ itakayozunguka kwenye mikoa ya Tanzania.
Akiongea na mtangazaji Dj Magasha kwenye kipindi cha Track 2 Track cha Fadhila FM ya Masasi, Ben Pol amesema kuwa baada ya mwezi wa Ramadhan anatarajia kufanya ziara ya ‘Moyo Mashine’ na hana mpango wa kuachia wimbo mpya kwa sasa.
“Kwa sasa hivi nataka kufanya ‘Moyo Mashine Tour’, nasubiri mwezi wa Ramadhan umalizike ili niupeleke ‘Moyo Mashine’ mikoani. Bado sijafikiria kuachia wimbo mwingine mpya kwa sasa ila nimefocus zaidi kufanya ziara ya ‘Moyo Mashine,” alisema.
Kuhusu kufanya video Afrika Kusini, muimbaji huyo alisema, “Sababu ni nyingi, kwa mimi binafsi nilienda kutafuta ubora wa picha kutokana na kitu fulani hivi niliona nitakipata cha ziada. Lakini pia upatikanaji wa vitu vyote unavyovitaka kwenye video ikiwemo magari na mazingira tofauti.” 
“Lakini kubwa kuliko vyote ni connection, kwa sababu ukiwa unafanya kazi kila siku na watu wako wanakuwa ni wale wale unakuwa haukuwi. Unavyoongeza watu na connection inaweza ikakusaidia na wewe ukakua zaidi,” aliongeza

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search