Thursday, 30 June 2016

SNURA AKUMBWA NA MAJANGA TENA VIDEO YAKE YAKATALIWA TENA

June 30/06/2016 at 10:02 am


Mwezi na nusu uliopita, Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo iliifungia video ya wimbo huo na kumwagiza Snura awasilishe script mpya ambayo hata hivyo baada ya kufanya hivyo nayo imekataliwa.
 Snura alidai kuwa baada ya bodi hiyo kukaa kwenye kikao iliona kuwa bado script mpya inataka kufanana na video iliyopigwa marufuku na kumkataza kushoot.
Amedai kuwa jibu hilo lilimchanganya na kumrudisha nyumba na kwamba video ya pili alipanga kuwepo mwenyewe na wala hatocheza zaidi kutembea.
‘’Nilipeleka script a video mpya ta Chura bodi ya filamu ilichukua muda kidogo kuipitia nilifuatilia sana ndio nikapewa majibu baada ya wao kukaa kikao na kupitia wakaniambia kuwa ile script hwajaikubali nishuti kwasababu wanasema maudhui yake yanataka kufanana na ile video ya mwanzo.
Nilishindwa kuelewa kwasababu kwa uelewa wangu niliona nimeandika kitu tofauti kwasababu video ya mwanzo ilikuwa imechezwa kwenye maji na wanawake ndio walikuwa wanacheza lakini video hiyo ambayo niliyokuwa nimeiandika ilikuwa ni mimi mwenyewe ndio nitakuwepo kwenye hiyo video halafu sichezi natembea huku naimba.
Halafu watu wananiona mie natembea huku naimba na wao wananifuata kwa nyuma huku wanacheza naenda napanda daladala na wao wanapanda nikishuka na wao wanashuka huku wakicheza’’ Alisema Snura

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search