Friday, 15 July 2016

JERRY MURO AAMUA KUSALIMU AMRI AKUBALIANA NA ADHABU ALIYOPEWA NA TFF


Afisa habari wa klabu ya Yanga Bw. Jerry Muro ameamua kukubali hukumu iliyoolewa dhidi yake na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayomtaka kutojihusisha na masuala ya soka kwa muda wa mwaka mmoja.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa instagra, Muro ame-post ujumbe unaoashiria ameamua kuukubali uamuzi huo huku akisisitiza atawa-miss mashabiki wake wa Yanga.
IMG_201607195_105109

“Kila nikifikiria figisu za soka la Bongo aisee nachoka kabisa, let me walk away for a while though I will be missing my fans and my people wa kimataifa but I must walk away for a while,” ndivyo inavyosomeka post ya Muro kwenye account yake ya instagram.

Kamati ya nidhamu ya TFF ilimtia hatiani Jerry Muro kwa kosa la kupinga uamuzi wa TFF na kulishambulia kupitia vyombo vya habari shirikisho hilo la soka nchini ambapo kamati hiyo ilitoa adhabu ya kumfungia Muro kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja pamoja na faini ya shilingi milioni tatu za Tanzania.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search