Saturday, 2 July 2016

MKUU WA WILAYA YA MBOZI AAMUA KUJIUZULU SIKU CHACHE BAADA YA KUTEULIWA

July 02/07/2016 at 2:22 pm

Mkuu wa Wilaya (DC) Mteule wa wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, Ally Masoud Maswanya ametangaza kujiondoa katika nafasi hiyo ya ukuu wa wilaya.
Kufuatia kujiondoa huko kwa Ally Masoud, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kongwa, John Ernest Palingo anakwenda kuwa mkuu wa wilaya ya  Mbozi, na Kongwa itasubiri uteuzi mpya utakaofanya na Rais Magufuli.
Sababu ya kujiondoa katika nafasi hiyo bado haijawekwa wazi lakini watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Tanzania wamekuwa wakisema maslahi ya kifedha ya utumishi wa umma kama Mkuu wa Wilaya ni madogo ukilinganisha na nafasi yake katika kampuni ya Tigo ambapo wastani wake wa mshahara kwa mwezi ni zaidi ya shilingi milioni 10 za Kitanzania pamoja na faida nyingine nyingi katika taaluma yake.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search