Friday, 8 July 2016

NUHU MZIWANDA:-SIWEZI KUINGILIA BIFU LINALOENDELEA KATI YA SHILOLE NA VIDEO QUEEN WA JIKE SHUPA

Mkali wa wimbo ‘Jike Shupa’ Nuh Mziwanda amesema hawezi kuingilia bifu ambalo limezuka kati ya aliyekuwa mpenzi wake Shilole na video queen wa video yake ya ‘Jike Shupa’ aitwae ‘Zuu’
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa yupo chini ya label ya ‘LFLG’, ameiambia ubuyu kuwa kwa sasa hawezi kuingilia ugomvi usiyomuhusu.
“Wale ni wanawake kwa hiyo zile ni tofauti zao, siwezi kuingilia na siwezi kuongea chochote, yule demu mimi nilimlipa pesa yake ya video akafanya, kazi yangu kamaliza masuala yake yanayoendelea kimpango wake,” alisema Nuh.
Aliongeza, “Kwa hiyo siwezi kuingilia na wala sitaki kufuatilia na wala sitaki kujua kwa sababu nimeshamalizana nae. Yale ni maisha yake binafsi siwezi kuingilia,”
Shilole na video queen wa video ya ‘Jike Shupa’ wamekuwa wakitupia vijembe katika mitandao ya kijamii.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search