Monday, 18 July 2016

SOMA UJUMBE HUU NI MUHIMU SANA KWA WANAUME WALIOOA

MPUMBAVU,narudia tena,MPUMBAVU,kama Mwanaume anayeweza kusahau fadhila za Mdada aliyemvumilia kwenye shida,akiwa kapuku maji,ana ndevu tu Wallet haina hata hela ya kwenda salon kushave,mpaka leo umefika hatua ambayo hao Wadada wengine wanakuona Mali,coz unavutia na Kupendeza,halafu unamsahau Mtu aliyekuvumilia from Scratch,akakuweka hapo ulipo,Kwa uaminifu hata pale alipokuwa na sababu 90,000 za kukusaliti lakini hakufanya hivyo,akajitunza kwa ajili yako coz anakupenda kweli.Leo hii,umesahau yooteee,umesahau alilia mara ngapi kwa ajili yako akakusamehe,mara ngapi uliukwangua moyo wake kama vocha ya jero,lakini akapona akasamehe,Unamuacha bila sababu ya msingi kisa umekatikiwa vizuri kwa wiki 2 na kicheche ambaye kesho na keshokutwa ukifulia atakuacha na kurukia mwanaume mwingine mwenye good look na pesa.
Wanawake wa mji huu wanajiposition kutokana na Hali yako ya Sasa..Hawajui Umefikaje hapo na Nani kakufikisha,waowanadandia tu....
Heshimuni Wadada waliowavumilia na kuwafanya Muwe Wanaume mnaong'aa leo...Mnajisahau sana..Na huu ni UPUMBAVU...Kumbuka ulikotoka,Vicheche wapo na saizi yao ni kuiba vifaranga vya kuku lakini sio kukuiba wewe Mwanaume mzima na akili zako...

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search