Monday, 18 July 2016

UMOJA WA AFRIKA WAZINDUA PASSPORT MOJA YA KUSAFIRIA

AU yazindua hati ya kusafiria na kufanikiwa kufufua ndoto za mmoja wa waliokuwa wakereketwa wa Umoja huu wa Afrika Hayat Muamar Gadaff ambaye alipinduliwa na kuuawa mwaka 2011.


Katika ndoto zake Gadaf alitamani afrika kuwa moja kiutawala kwa kuwa na rais mmoja na kwa kaunza tayari Umoja wa  Afrika AU umezindua Pass ya kusafiria moja.
Image captionBara la Afrika limezindua rasmi cheti chake cha kusafiria!
Je unamiliki hati ya kusafiria ya taifa lako?
Hivi Karibuni, utakuwa huhitajiki kusafiri katika nchi za kiafrika kwa hati nyingine kwa kuwa wewe ni mwafrika !
sababu kubwa hasa Bara la Afrika limezindua rasmi cheti chake cha kusafiria!
Madhumuni ya AU umoja wa Afrika kuzindua cheti hicho ni kuvunja mipaka iliyowekwa na mkoloni alipoigawanya Afrika ilikuitawala katika karne iliyopita.
Image captionViongozi wa kwanza kupewa cheti hicho ni rais mwenyeji wa kongamano hilo Paul Kagame wa Rwanda na mwenzake wa Chad rais Idris Deby.
Viongozi wa kiafrika wamezindua cheti hicho maalum mjini Kigali Rwanda katika kongamano la viongozi wa Afrika.
Wakwanza kupewa cheti hicho watakuwa ni viongozi wenye hadhi ya kupewa vyeti vya kidiplomasia.
Viongozi wa kwanza kupewa cheti hicho ni rais mwenyeji wa kongamano hilo Paul Kagame wa Rwanda na mwenzake wa Chad rais Idris Deby.
Image captionMadhumuni ya AU umoja wa Afrika kuzindua cheti hicho ni kuvunja mipaka iliyowekwa na mkoloni alipoigawanya Afrika ilikuitawala katika karne iliyopita.
Marais wote waliohudhuria kongamano hilo watapewa cheti hicho cha AU kabla ya kukamilika kwa mkutano huo.
Mawaziri wa maswala ya kigeni na viongozi wakuu katika umoja wa Afrika pia wanatarajiwa kufaidi cheti hicho cha kusafiria.
Umoja wa Afrika unatarajia kuwa mataifa ya kiafrika yataanza kutoa vyeti hivyo vipya vya usafiri kufikia mwaka wa 2018.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search