Wednesday, 26 October 2016

HAYA NI MAJINA YA WALIOFANIKIWA KUPATA MKOPO AWAMU YA KWANZA


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imetangaza awamu ya kwanza ya majina ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini watakaopewa mkopo kugharimia masomo yao.

Idadi ya wanafunzi ambao tayari wamepitishwa kupata mkopo ni 7,904, hata hiyo imeelezwa kiwango hicho kitaendelea kubadilika kwa kuwa mchakato unaendelea.

Taarifa iliyotolewa jana na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Stella Manyanya ilibainisha kuwa bodi imekamilisha uchambuzi wa majina ya waombaji ambao wana sifa zinazotakiwa na majina ya wanufaika wapya ambayo yameanza kutangazwa kupitia tovuti ya bodi hiyo.
Kuona majina ya wanafunzi waliopata mkopo kwa awamu ya kwanza bonyeza hapa –>> HESLB 2016/17

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search