Wednesday, 22 March 2017

SERIKALI YAMKANA MANJI MAHAKAMANI KUWA HAIJAWAHI KUMSHIKILIA

Sakata la mfanyabiashara Yusuf Manji kushikiliwa na polisi kwa muda wa siku 28 katika Hospitali ya Agha Khan limezua sura mpya baada ya Jamhuri kukana kwa kiapo kuwa haikuwa inamshikilia mfanyabiashara huyo.
Madai haya yalifikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam mbele ya Jaji Ama-Isario Munisi, wakati maombi ya Manji kutaka aachiwe kizuizini anakoshikiliwa pasipo uhalali, kuanza kusikilizwa.
Mawakili wa Manji, Hudson Nduseyo, Alex Mgongolwa na Jeremiah Ntobesya walipeleka ombi hilo katika Mahakama Kuu wakidai kuwa mteja wao anashikiliwa isivyo halali, hivyo wanaiomba mahakama imwachie huru.
Majibu yaliyotoka kwa Wakili wa Serikali, Osward Tibabyekomya, aliyewasilisha majibu ya kiapo kinzani yalikinzana na maombi hayo.
Wakili wa Serikali alidai kuwa aliwasilisha mahakamani majibu ya viapo viwili kinzani, kimoja kikiwa kimeapwa na mpelelezi kutoka idara ya uhamiaji, Anorld Munuo na cha pili kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kilichoapwa na Salum Ndalama. Alidai kuwa katika viapo vyote viwili, waapaji wanasema Manji hashikiliwi na polisi wala uhamiaji.
Akijibu, Wakili Mgongolwa alidai kuwa Manji anashikiliwa na idara ya uhamiaji na analindwa na polisi kwa muda wa siku 28 sasa.
“Mheshimiwa jaji, hata leo Manji kaletwa chini ya ulinzi, askari wamemfikisha mahakamani wenyewe wakakaa nje. Mara ya kwanza walitumia gari langu.. hata leo walitaka kutumia gari langu lakini wakaamua kumleta na gari lao.”
“Mheshimiwa jaji Manji analindwa na polisi sita, tunaomba tupewe muda wa kujibu majibu ya kiapo kinzani na iwekwe kwenye kumbukumbu za mahakama kwamba hashikiliwi kama wanavyodai jamhuri.”
Aliendelea kusema “Sisi hatuwezi kuwa wendawazimu tulete maombi mahakamani kuomba aachiwe kizuizini wakati hajashikiliwa”
Jaji Munisi naye alisema kuwa majibu ya kiapo kinzani yote mawili yanaeleza kwamba Yusuf Manji hajashikiliwa. Na alishangazwa na kutofautiana kati ya pande hizo mbili.
Alisema “Nashangaa, najiuliza maswali  kwa nini jamhuri wanasema hawajamshikilia na waleta maombi wanasema anashikiliwa..!!

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search