Monday, 29 May 2017

ANGALIA LIVE IGP MPYA SIMON SIRO AKIAPISHWA IKULU JIJINI DAR

Habari waungwana,

Kama tujuavyo, jana Rais Magufuli alifanya mabadiliko kwenye jeshi la polisi nchini kwa kutengua uteuzi wa aliyekua mkuu wa jeshi hilo, Ernest Mangu nafasi ambayo alitumikia kutoka awamu ya nne alipoteuliwa na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.

Nafasi yake kukabidhiwa Simon Sirro ambae alikuwa kamanda wa polisi mkoa wa Dar-es Salaam, uteuzi ambao alipewa na Rais wa sasa, John Magufuli.

Kwa sasa unapigwa wimbo wa Taifa na watu kadhaa wamehudhuria ikiwemo makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na IGP anaeachia nafasi hio, Ernest Mangu.

VIDEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Mei, 2017 amemuapisha Kamishna wa Polisi Simon Nyakoro Sirro kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).
Hafla ya kuapishwa kwa IGP Simon Nyakoro Sirro imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Gerson John Mdemu, Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, Makatibu Wakuu wa Wizara na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Bw. Paul Christian Makonda.
Kabla ya IGP Simon Nyakoro Sirro kuapishwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Mhe. Rais Magufuli amemvua cheo cha zamani cha Kamishna wa Polisi na kumvalisha cheo kipya cha Inspekta Jenerali wa Polisi.
Katika hafla hiyo IGP Simon Nyakoro Sirro, pia amekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Katibu wa Utumishi wa Umma kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. John Marko Kaole.
IGP Simon Nyakoro Sirro amechukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search