Friday, 26 May 2017

AWATAKAO FANIKISHWA KUKAMTWA KWA WATUHUMIWA WA MAUAJI KIBITI KIBITI KULIPWA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limetangaza zawadi ya Tzs. milioni 5 kwa mwananchi ambaye atafanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa 12 ambao limedai wanajihusisha na mtandao wa mauaji yanayoendelea katika Wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Onesmo Lyanga, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Jeshi hilo linaendelea kuwasaka watuhumiwa hao.
Alisema Polisi imepata picha za baadhi ya watuhumiwa na fununu za mahali wanapopenda kutembelea mara kwa mara.
Kamanda Lyanga aliwataja watuhumiwa hao pamoja na mwanzilishi wa mtandao huo wa mauaji kuwa ni Abdurshakur Ngande Makeo, Faraj Ismail Nangalava, Anaf Rashid Kapera, Said Ngunde na Omary Abdallah Matimbwa.
Wengine ni Shaban Kinyangulia, Haji Ulatule, Ally Ulatule, Hassan Uponda, Rashid Salim Mtulula, Sheikh Hassan Nasri Mzuzuri na Hassan Njame.
“Jeshi letu limewabaini watuhumiwa hao kwa kushirikiana na wasiri wetu huku tukiendelea na uchunguzi zaidi,”alisema Kamishna Lyanga.
Alisema polisi imegundua kuwa watuhumiwa hao hupendelea kutembelea maeneo ya kisiwa cha Simbaulanga, kisiwa cha Saninga katka kijiji cha Nchinga na kijiji cha Mfesini kata ya Nyamisati pamoja na maeneo mbalimbali ya wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga.
Kamishna Lyanga aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wa kuwafichua watuhumiwa wote wa mtandao ambao unahatarisha hali ya usalama mkoani hapa.
Mauaji ya raia na hasa viongozi wa kisiasa katika wilaya hizo za mkoa wa Pwani yalianza kama utani Aprili 30 mwaka jana alipopigwa risasi mwenyekiti wa kijiji, Said Mbwana kabla ya kushika kasi na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 30 wakiwamo polisi.
Kiongozi wa mwishoni kuuawa ni aliyekuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Bungu wilayani Kibiti na mkoani Pwani, Arife Mtulia wiki iliyopita.
Mtulia aliuawa nyumbani kwake na watu wasiojulikana ambao hawakuchukua chochote wakati akienda kuoga usiku.
Kifo cha Mtulia kimekuja huku kukiwa na operesheni kabambe ya kusaka majambazi yaliyoua polisi nane katika eneo la Mkengeni, Kata ya Mjawa katikati ya mwezi uliopita.
Polisi inaendesha kimyakimya operesheni hiyo kwa hofu ya kuanika kinachofanywa na kikosi cha operesheni katika kuchunguza tukio hilo.
Operesheni hiyo inayoendelea kwenye mapori na maeneo mengine inahusisha vyombo vya ulinzi na usalama

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search