Tuesday, 30 May 2017

BANDA AFUNGUKA SABABU ZINAZOMFANYA AONDOKE SIMBA


Mlinzi kiraka wa klabu ya Simba Abdi Banda amesema anaondoka klabuni hapo kwa kuwa makataba wake umeisha na hakuna mazungumzo yanayoendelea kati yake na uongozi wa wekundu hao, hadi sasa.

Banda, aliwashukuru mashabiki wa Simba na kuwaaga kwenye ukurasa wake wa Instagram, mara baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Mbao na kutwaa kombe la TFF Uwanja wa Jamhuri Dodoma, Jumamosi iliyopita.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Dodoma, Banda amesema viongozi wa Simba hawaoneshi kumuhitaji kwani hawajazungumza naye hadi sasa.

"Ni kweli naondoka kwa sababu mkataba wangu umeisha na hakuna kiongozi aliyezungumza na mimi kuhusu mkataba mpya, na ndo maana niliwaaga mashabiki wa Simba kwenye Instagram". Alisema mlinzi huyo wa zamani wa Coastal Union.

Kuhusu wapi anaelekea kwa maisha mapya ya soka, Banda alisema kuwa anataka kuelekea Afrika Kusini kucheza soka huk

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search