Monday, 29 May 2017

BEKHAM ATUA NCHINI KIMYA KIMYA

Taarifa za uhakika ni kuwa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Real Madrid, LA Galaxy na PSG pamoja na timu ya taifa ya England, David Beckham yupo nchini Tanzania.
Picha ya video ambayo imemnasa staa huyo akiwa na wanaye, imemuonyesha akitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, ambapo alipitia mlango wa watu maalum (VIP) huku akiwa amemshika mkono mtoto wake wa kike.
Katika msafara huo ambao ulioonyesha wazi kuwa Beckham hakutaka purukushani za waandishi wa habari, watoto wake wa kiume watatu walikuwa mbele huku wakizungumza na kuongozwa na msaidizi wa uwanjani hapo.
Mkewe, Victoria Beckham alikuwa nyuma yao huku naye akitembea kwa kasi.
Haijajulikana sababu za ujio wa staa huyo na familia yake.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search