Monday, 22 May 2017

BINTI ACHA KUPIGA MIZINGA KWA KUFANYA HIVYO UNAJIPOTEZEA BAHATI YAKO


NENO KUPIGA KIZINGA NI NENO LA KAWAIDA ILA USICHOJUA UPIGAJI WA VIZINGA NI HATARISHI KWA MAHUSIANO HASA VIZINGA VISIVYO NA MSINGI.
Mabinti wengi wanajisahau sana katika hili na ndio mana unaweza shangaa mwanaume wako ghafla anaanza kukukimbia unajiuliza nimekosea wapi kumbe umekosea kwenye vizinga kuomba vitu vya ajabu ajabu.Unaweza shangaa ulikuwa na mwanaume unaomba hela za ajabu ajabu anakupa ila ukashangaa kakuacha kawa na mtu mwingine wamekaa baada ya muda unashangaa mwenzio ambaye kachukua nafasi yako amepewa kitu cha thamani ambacho hukuwahi hata kukiwaza.

Acha nikuambia vizinga vya kipuuzi ni vipi hasa.Mmeanza mna wiki mbili tu ushaanza baby mwenzangu yani hili wigi nishalichoka naomba hela nikasuke baby wangu,mara jamani baby mwenzio kuna gauni nimeliona nimelipenda bei yake 17,000 naomba baby wangu nikanunue,Hajakaa vizuri boo nikuambie kitu wiki ijayo kuna birthday ya rafiki yangu nataka nimnunulie keki japo ya 20,000 plz baby nisaidie hivi ndio vizinga vya kipuuzi na vingine vingi.Leo hii kirahisi unapiga vizinga vya vocha kila wiki mtu akuungie bando ndio vizinga vyako.Acha nikuambie binti hakuna mwanaume ambaye anapenda kuwa na mwanamke ambaye ni omba omba hasa wa vitu ambavyo havina msingi.
Mwanamke shujaa mwenye kujielewa haombi ovyo bali anapotaka kuomba kitu anaomba kitu ambacho kina direct impact katika maisha na ambacho kimeshiba na sio kukiomba kila mara.Unaweza kuwa na mwanamke ukashanga mna muda na hakuombi vitu hovyo the day anakuja kukuomba anakuomba kitu ambacho hata mwenyewe ukipima kumsaidia kwake namna moja utakuwa na wewe umejipa msaada katika maisha yako kama wapenzi.

Halafu acha niwape siri ukiomba mwanaume wako kitu usikurupuke kaachini uandae kama proposal kabisa yani unampa uchanganuzi wa kile unachoomba na kwanini unaomba ili kuonesha wazi huombei tamaa.

NAOMBA NIKUAMBIE KABISA BINTI HIVYO VIZINGA VYA MABANDO NA HELA ZA MAWIGI ZA KILA WIKI ZITAKUFANYA UKIMBIWE.JIFUNZE KUJIZUIA KWA VITU AMBAVYO HAVINA MSINGI NA UNAPOTAKA KUOMBA KITU OMBA KITU AMBACHO KINAONEKANA KINA IMPACT NA MAISHA.

UTASHANGAA UMEKAA NA MWANAUME MIAKA SIKU UNAACHWA HUNA CHOCHOTE ULICHOPATA ZAIDI YA KUBADILI STYLE ZA MAWIGI TU.

#TheOceanOfLove

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search