Saturday, 6 May 2017

CCM YASEMA HAYA JUU YA KUPOTEA KWA KINANA


Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa Katibu mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana alikuwa akiugulia afya yake pindi yupo kazini hivyo alichukua muda wa kutosha kwenda nje ya nchi kupatiwa matibabu.

Polepole amezungumza na AZAM NEWS ambapo alisema tangu Mzee Kinana akiwa hata kwenye mkutano mkuu wa CCM Dodoma hakuwa sawa kiafya.

“Tangu akiwa kwenye mkutano mkuu maalumu wa CCM Dodoma hakuwa sawa kiafya, alikuwa anafanya yote haya akiugulia afya yake kwahiyo ikakubalika achukue muda wakutosha wa kuitizama afya yake nje ya nchi na anapo rejea mgonjwa akitoka hospitali huwa hakimbii kazini, shambani moja kwa moja inashauriwa kitaalam atumie muda wa kupumzika ili kuimarisha afya yake na nimezungumza nae anaendelea vizuri yuko madhubuti kabisa kuliko jana,” alisema Polepole.

Katibu mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana hajaonekana hadharani kwa muda tangu Rais Magufuli aliposema kuwa yuko India

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search