Tuesday, 30 May 2017

CHONDE CHONDE MWANAUME,USIMUULIZE MWANAMKE MASWALI HAYA MATANO

Kuna maswali mengi ambayo ukimuuliza tu mwanamke, hutia doa uhusiano, yaepuke ili kulinda uhusiano wako mzuri. Maswali hayo ni haya yafuatayo:

1.    NIAMBIE KUHUSU MPENZI WAKO WA ZAMANI:

Usimuulize hili swali kabisa kwa sababu linaweza kumrejeshea kumbukumbu zenye kuumiza ambazo zitamfanya awe na tahadhari zaidi dhidi yako au akaanza kukulinganisha na mpenzi wako wa zamani.

2.    UNA MIAKA MINGAPI?

Utampa tabu sana utakapomuuliza swali hili, na iwapo atakuwa na umri mkubwa kidogo atapata shida sana. Usifanye haraka kumuuliza hilo, jibu lake utalipata baadaye.

3.    UZITO WAKO?

Jihadhari sana kumuuliza kuhusu uzito wake, kwani atalielewa kivingine kabisa. Kumuuliza hivyo ni sawa na kumwambia: “Wewe ni mnene”.

4.    JE, WANIPENDA?

Maswali yanayojibiwa kwa “Ndiyo au Hapana” humkera sana mwanamke. Swali kama “je, wanipenda?” humkera. Hata kama anakupenda lakini anaficha hisia zake, hatoziweka wazi kwa urahisi hivyo, kwani mwanamke anapenda mwanaume anayeongoza uhusiano.

Mwanamke akipenda, vitendo hutawala kuliko maneno. Ikiwa unahisi kuwa anakupenda tu, basi mwambie hivyo bila maswali.

5.    KWA NINI HUJAOLEWA?

Sijui unakusudia nini kuuliza swali hili. Je, unakusudia kwamba ni mbaya au hafai kuwa mke?

Hakuna sababu ya kuuliza swali hili, jiepushe nalo kabisa, utamkera sana

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search