Monday, 8 May 2017

CNN na Al Jazeera zaripoti ajali iliyoua 32 Tanzania


Ajali iliyoua watu 32 kwa mkupuo nchini Tanzania wakiwemo Wanafunzi watoto 29 wa shule ya St. Lucky Vicent na watu wazima watatu wakiwemo Waalimu na Dereva, ni habari kubwa sio tu Tanzania bali hata kimataifa.
Vituo vya TV vya kimataifa vya CNN na Al JAZEERA ni miongoni mwa vyombo vya habari vya kimataifa vilivyorusha habari hii kwenye TV na hata kwenye mitandao yao kama inavyoonekana hapa chini.
Watoto hao pamoja na Waalimu wao wanatarajiwa kuagwa kwenye uwanja wa mpira Sheikh Amri Abeid Arusha Jumatatu asubuhi ya May 8 2017 na shughuli hiyo itaongozwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu.
.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search