Tuesday, 16 May 2017

HAYA NDIYO MAISHA HALISI YA WAZEE WETU HUKO VIJIJINI

Image may contain: one or more people, people standing, plant and outdoor
Haya ndiyo maisha halisi ya wazazi wetu huko kijijini, lakini vijana tukifika mijini tunasahau kila kitu na kujifanya sisi ni wa kimataifa. Miadi yetu inakuwa samaki samaki, Mlimani city, Soccer city na viwanja mbali mbali huko mjini.
Siku unaambiwa Baba Mama yako amaaga dunia hata nyumba yakuingiza jeneza hakuna ulijisahau mjini kwa kuitwa BABY, HUBY, SWEET na majina kadha wa kadha huku wazazi wako wakipambana na jembe la mkono mpaka mwisho wa maisha yao.
Tukumbushaneni ndugu zangu hili jambo hata Mimi linanihusu, maana hata Mimi nimetoka huko kijijini. Hasa nyinyi Dada zetu mkifika huku mjini ulikuwa Unaitwa NYANJIGE, NYANZURA, ROBY,NYANGERE leo haushikiki vile vile na akina kaka pia wote pipa na mfuniko.
Kumbuka kuna kukwama siku moja pengine umepoteza uwezo wakujisimamia labda kutokana na malazi unarudi kwenu unawakuta wazee wako ulio wasahau miaka dahari hawana kitu na wewe huna kitu what are you expect..?
Huwa namkumbuka sana Mheshimiwa Jakaya Kikwete alisema kajenge kwenu hata kibanda siku ukifa maiti yako isisumbuke.
Tafakuri.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search