Tuesday, 30 May 2017

HAYA NI MAMBO SITA AMBAYO MKE HAPENDI KUYAONA KWA MUME WAKE

Hizi ni sifa ambazo mke huchukia kuziona kwa mumewe:

1.    UBAKHILI: Miongoni mwa safi nyingi ambazo mke anaweza kuchukia kuziona kwa mume wake ni suala la ubakhili. Sambamba na ubakhili wa kipesa au vitu, mume anaweza kuwa bakhili wa kuelezea hisia zake kwa mke na kwa familia yake.

2.    UMIMI: Wakati fulani mwanaume hupendelea kufanya mambo kwa umimi bila kuzingatia hisia za mkewe au familia yake na mahitaji yao. Wakati mwingine mwanamke anashindwa kuvumilia tabia hii yenye kuudhi na humpendelea mwanaume anajitoa kwa ajili ya furaha ya familia yake.

3.    AHADI ZISIZOTIMIZWA: Mwanamke anamchukia mwanaume anayeahidi bila kutekeleza alichokiahidi.

4.    UBABE: Mwanamke hapendi kuishi na mwanaume mbabe na anayetumia mabavu katika maisha yake yote. Daima mwanamke humpenda mwanaume anayemheshimu na kumuunga mkono katika maisha, sio mwanaume mbabe, mbinafsi na anayetaka kutumia mabavu yake.

5.    WIVU ULIOPITILIZA: Mwanamke hapendi kuishi na mwanaume ambaye muda wote anamuonea wivu na kumshuku kupitia kiwango. Sifa na tabia hii inaweza kuzorotesha uhusiano wa kindoa.

6.    URONGO: Mwanamke hampendi mwanaume dhaifu anayeogopa kusema ukweli, na anayemuongopea ili kuficha makosa na kasoro zake. Hivyo, inapendeza zaidi mume akiwa muwazi kwa mke, japo wakati fulani huwa na ugumu, kwa sababu hilo litamfanya apate kuheshimiwa na mkewe. Kama ambavyo ukweli husaidia kuondosha mikingamo baina ya wanandoa, kadhalika urongo huyafanya matatizo yao kuwa magumu zaidi.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search