Monday, 8 May 2017

HII NI REKODI ALIYOIWEKA ARSENE WENGE BAADA YA KUMFUNGA MOURINHO

Jumapili ya May 7 2017 Arsenal imecheza na Man United kwa mara ya 225 toka timu hizo zikutane kwa mara ya kwanza October 13 1894 katika mchezo wa Division League uliomalizika 3-3, kabla ya mchezo wa leo Arsenal ilikuwa imeifunga Man United mara 81 na kupoteza mara 96 sare zikiwa mara 47.
Game yao ya May 7 2017 Arsenal chini ya Arsene Wenger imeifunga Man United 2-0 kupitia kwa Xhaka na shuti la nje ya box dakika ya 53 na Danny Welbeck aliyefunga kwa kichwa dakika ya 56 na kuifanya Arsenal kuwa timu pekee EPL iliyofunga magoli mengi ya vichwa msimu huu, imefunga jumla ya magoli 15 kwa vichwa.
Ushindi huo ndio umekuwa ushindi wa kwanza kwa kocha Arsene Wenger dhidi ya Jose Mourinho katika Ligi Kuu EnglandWenger hakuwahi kumfunga Jose Mourinho katika Ligi kuu England na unaambiwa kabla ya leo, Wenger alikutana na Mourinho mara 12 katika EPL na kufungwa mara 7 na sare mara 5.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search