Wednesday, 17 May 2017

HILI HAPA TAMKO LA CHADEMA BAADA YA RAIS MAGUFULI KUIVUNJA CDA


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya kati kimeitaka serikali kuwalipa fidia wakazi wa Manispaa ya Dodoma ambao kwa namna moja au nyingine wameathirika  wakati Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) ilipokuwa ikifanya kazi kwa kuporwa ardhi yao.

Kauli hiyo imetolewa  na Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni wa Chadema, Benson Kigaila wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa.

Kigaila amesema kuwa Rais John Magufuli hawezi kuivunja CDA na ikawa ndiyo mwisho wake bila kuangalia madhara yaliyosababishwa na mamlaka hiyo kwa wananchi katika kipindi chote cha miaka 44 iliyofanya kazi.

Amesema fidia hiyo ni lazima ilipwe na serikali kuu ambayo ndiyo iliyoiweka CDA madarakani na siyo kuliachia jukumu hilo Manispaa ya Dodoma kwa kuwa haihusiki na unyang’anyi huo.

"Kuivunja CDA siyo hoja. Hoja inayokuja hapo ni je wananchi wa Dodoma walionyang'anywa ardhi yao na CDA bila kulipwa fidia watafidiwaje au ndiyo wataachwa waendelee na maumivu yao?" amesema Kigaila

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search