Tuesday, 9 May 2017

HILI NI AJABU LINGINE LA DUNIA

Katika Kisiwa binafsi cha  Fiji, Poseidon Resort, kuna hoteli ya nyota tano iliyojengwa chini ya bahari kiasi cha futi 12 hadi 40 katika eneo ambalo mtu anaweza kuona matumbawe na samaki wanaoishi humo.

Asilimia 70 ya vyumba vyake vinakuwezesha kuona waziwazi mazingira chini ya maji.
Ikiwa na vyumba vya kifahari 25  ina mambo yote ambayo hoteli inastahili kuwa nayo na mgeni aliyechoka kukumbana na samaki na matumbawe anaweza kushusha teknolojia stahiki ili kuzuia muono.

Yaani mtu ukiingia humu halafu unalala ukiangalia bahari ni kitu cha kutamanisha sana.
Pia aneo la kujipatia kinywaji linazingua sana.
Je unataka kufanya safari ya baharini? hautakuwa na shida kuna nyambizi za biashara ambazo zitaweza kuwatembeza wageni chini kwa chini.
Imeelezwa kuwa hoteli hii ni salama kwa kuwa ujenzi wake umechukua mfumo wa nyambizi za kubebea abiria.
Ukitoka hotelini hapo na unataka kufurahi unaweza kwenda kwenye kucheza gofu.
Hii hoteli haikutengenezwa kwa ajili ya mtu maskini ni kwa matajiri wachache kwani chumba kimoja kwa wiki ni dola za Marekani 15,000 na kama unataka kuwa na mwenzi wako katika mapenzi mubashara ujue kabisa utalazimika kulipa dola za Marekani 30,000.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search