Monday, 15 May 2017

HIVI NDIVYO UGUMU wa Maisha Unachochea Ongezeko la Upungufu wa Nguvu za Kiume

Habari wanajamii. Unaweza kujiuliza ni jinsi gani ugumu wa maisha unawezaje kuhusiana na upunguvufu wa nguvu za kiume? Basi ngoja nikufafanulie hili,
Upungufu wa nguvu za kiume umekuwa ni tatizo kubwa linaloikumba jamii kwa sasa.
Tafsiri halisi ya upungufu wa nguvu za kiume: Ni ile hali ya mwanaume/mwanamke (ambaye amesha balehe/kukomaa kimaumbile) kushindwa kumudu ipasavyo tendo la ndoa ikiwa ni pamoja na kushindwa kusimamisha uume vizur, kuwahi kufika kileleni, kushindwa kurudia tendo, kutofurahia tendo na mengine mengi yanayo fanana na hayo.

JINSI GANI UGUMU WA MAISHA UNAWEZA SABABISHA TATIZO HILI.
Kutokana na hali ya maisha ya sasa, yani maisha kuwa magumu kwa maeneo mengi nchini yaliyosababishwa na vitu vifuatavyo.

1. Mfumuko wa bei za bidhaa mbali mbali, 2. Tatizo la ukosefu wa ajira,
3. kutokuwa na ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi,
4.kupanda kwa gharama mbali mbali za huduma kama vile Afya, Usafir na Makazi.
5. Kupunguzwa na kufukuzwa kwa wafanyakazi umma na sekta binafsi.
Hivyo basi kutokana na haya yote..watu wengi wamekuwa na stress za maisha (msongo wa mawazo ) ambao husababisha mambo yafuatayo ambayo kwa ujumla wake husababisha tatizo hili.
1. Kukosa furaha wakati wote. Hivyo ni vigumu kupata hamu ya tendo.
2. Familia kufarakana kutokana kutotimiza majukumu yao ya kila siku.
3. Unywaji wa pombe kupita kiasi wakiamini kwamba ni njia sahihi ya kupunguza mawazo.
4. Kutopata lishe bora hvy kusababisha miili kukosa nguvu ya kutosha kuratibu mambo mbali mbali mwilini ikiwa ni pamoja na shughuliki via vya uzazi.

ANGALIZO.
Tunaiyomba serikali iweze kuliangalia tatizo hili kwa jicho la tatu. Kwani kuna uwezekano mkubwa wa kupungua kwa ongezeko la watoto wanaozaliwa nchini hali ambayi huleta mambo yafuatayo:-
1. Taifa kukosa nguvu kazi ya kesho ambalo ndio maendeleo ya taifa kwa miaka ijayo.
2. Nchi yetu bado ni changa mapori ni mengi kuliko makazi hivyo ili kuweza kupata maendelea hatuna budi kuzaliana kwa wingi ili kuweza kutumia ipasavyo maeneo yaliyo baki.
3. Kukosekana kwa wataalamu wa baadae kama vile madaktari, wakandarasi, wanauchumi n.k
4. Kukosa vipaji vipya kwani vipaji ni zawadi toka kwa Mungu ambavyo huvipata katika uzao..hivyo ni chanzo cha kudumaa na kuzolota kwa taifa hili masikini.
Maoni yenu wadau...

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search