Monday, 15 May 2017

HIZI NI DALILI TANO ZA MWANAMKE MCHEPUKAJI

Licha ya wanaume wengi kuwa na wanawake wengi muda mwingine, hawapendi mpenzi wao awe na mwanaume mwingine wakiamini kuwa kufanya hivyo atakuwa hajatulia. Wivu huu si kwa wanaume waliooa tu, bali hata wale wenyeuhusiano wa kawaida.
Kwa kipindi cha miaka ya nyuma tabia ya wanawake au wanaume kuchepuka (kutoka nje ya ndoa) haikuwa kawaida kutokana na maadili, lakini ukuaji wa teknolojia hasa ya mawasiliano pmaoja na kasi ya utandawazi kumefanya kuchepuka kuwa jambo la rahisi na pengine linalochukuliwa katika hali ya ukawaida sana.
Zamani ilikuwa mwanamke akishaolewa basi anatulia kwenye ndoa yake hata kama kuna mapungufu atajitahidi kuyatatua akiwa ndani na si kuchepuka kwa kisingizio kuwa mumewe hamridhishi, au sababu nyingine.
Zifuatazo hapa chini ni baadhi ya tabia anazoweza kuzionyesha mwanamke ambaye anachepuka;
1. Anawahi kukasirika
Ukiona mwanamke anaanza kukasirika haraka hata kwa mambo yasiyo ya msingi, huenda ni dalili kuwa anachepuka. Atakuwa akikukasirikia na kuamua kutokukusemesha kwa mambo hata yasiyokuwa ya msingi.
Kiufupi hapa, mwanamke ambaye anachepuka ataanza kuonyesha tabia za tofauti na zile za awali kwa sababu mapenzi yake tayari ameyahamishia kwa mtu mwingine. Kama hajaanza kuchepuka basi anatafuta sababu ya kugombana na wewe ili aweze kuchepuka.
2. Dharau
Mwanamke ambaye ameanza kuchepuka/kuwa na uhusiano na mtu mwingine hushindwa kujizuia kumuonyesha mwenza wake dharau. Huwa hamjibu mwenza wake kitu kwa utaratibu na akisema kitu usiposikia ndio imetoka hivyo, sababu huwa hawarudii kitu.
Kila utakachomueleza ataona kama unamtesa na kuanza kuhoji kwanini wewe hufanya kana kwamba umemona yeye ni mtumwa wako. Hii itapelekea kuanza kutokukusikiliza kama ilivyokuwa awali.
3. Marafiki wengi wa kiume
Ikifikia hatua hii wewe jiongeze tu. Unakuta mpenzi wako au mke ana marafiki wengi wa kiume wengine ni waume za watu na wengine wahuni ukimuuliza, anakuuliza kwani kuna shida gani?
Mwanamke ambaye ana marafiki wengi wa kiume inakuwa ni rahisi kwake kuchepuka. Hii haimaanishi kuwa mwanamke hatakiwa kuwa na rafiki wa kiume, lakini kila kitu kiwe kwa kiasi na pia aina ya marafiki hao ni ya kutiliwa maanani.
Anaweza asiwe na uhusiano na wanaume hao lakini kadiri wanavyoendelea kuwa pamoja, uwezekano wa yeye kukusaliti ni mkubwa sana, hivyo ni vyema kuchukua tahadhari mapema kwa mkeo au mpenzi wako. Wakianza kumsifia na kumpa vijizawadi kuliko unavyofanya wewe, mwisho wa siku ukurasa unafungwa.
4. Anapenda vitu vya juu
Wanawake wanaopenda vitu vya bei ya juu ni wa rahisi kudanganyika na kuwasaliti waume zao. Wanawake wa aina hii huwa hawaridhiki na mahitaji wanayopewa na waume zao na wanaanza kutafuta vitu vya ziada nje na mwisho wa siku wanatumbukia kwenye vishawishi.
Na hii tabia ya kupenda vitu vya juu wakati mwingine huchangiwa na jinsi anavyowaona rafiki zake wanavyotumia vitu hivyo. Kwa vile mpenzi/mume wake hawezi kumgharamia, basi anaamua kuchepuka ili avipate.
5. Ana marafiki ambao ni michepuko
Kuna usemi unaosema ndege wafafanao huruka pamoja au ukikaa karibu na ua ridi utanukia. Hii ina maana kuwa kama mkeo/mpenzi wako hana tabia ya kuchepuka lakini akikaa karibu na wanaochepuka, basi kuna uwezekano mkubwa na yeye akaanza tabia hiyo kutokana na yale anayoyaona na kusikia.
Ukiona mke wako au mpenzi wako anaanza kukupigia stori za rafiki zake wanaochepuka, mwambie aache mara moja kuambatana nao.
Mbali na hizi, kuna dalili nyingi za mwanamke anayechepuka kwani kwa asilimia kubwa mambo hayatakuwa kama yalivyokuwa awali. Ni vema kuwa karibu na mwenza wake karibu ili ukiona dalili ya jambo ambalo halipo sawa muweze kujadiliana na muwe na uhusiano wenye afya

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search