Monday, 15 May 2017

KAULI YA MANARA YAZUA GUMZO MITANDAONI

Msimu wa 2016/17 unaelekea mwishoni, mbio za ubingwa zipo kwa Simba na Yanga lakini kitakwimu Yanga ndiyo wenye nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.
Yanga ina pointi 65 sawa na Simba lakini, Yanga ipo kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na kuwa ina wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa, pia ipo nyuma kwa mchezo mmoja zaidi ya Simba.
Wakati hali ikiwa hivyo, mitandaoni kumeanza kutembea video ya Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara ambaye alinukuliwa akijinadi mbele ya waandishi wa habari kuwa wamtafute baada ya miezi minne au mitano wamuulize juu ya ubingwa wa ligi kuu msimu huu ambao utakuwa mikononi mwa Simba.

Katika video hiyo Manara anasikika akisema: “Nitafuteni baada ya miezi minne au mitano niulizeni hili swali, mimi ninachoamini bingwa w amsimu huu ni Simba Sports Club, kwa dhati ya moyo wangu, ninaamini hivyo kwa kuwa najua tulivyojiandaa.”

Kutokana na tambo hizo, mashabiki wengi hasa wa Yanga ndiyo ambao wamekuwa mstari wa mbele kusambaza video hiyo kwenye mitandao ya kijamii kwa lengo la kutaniana kama ilivyo kawaida ya mashabiki wa pande hizo.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search