Tuesday, 9 May 2017

LEMA AWASHA MOTO BUNGENI


Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ameomba muungozo wa Spika wa kuhusu  ubaguzi wa kisiasa uliotokea kwenye msiba mjini Arusha Jana.

Jana Arusha ilikuwa inaagwa  miili ya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa Shule ya Lucky Vincent waliopoteza maisha katika ajali ya gari.


Lema amesema hata magari mawili ya kubeba wagonjwa yaliyotolewa na yeye na mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari yaliondolewa kwa sababu yana majina yao.

Amesema ni kwa sababu walimheshimu makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, vinginevyo mambo kama hayo huwa hayatokei mbele yao.

Mwenyekiti wa Bunge  Najma Giga amesema atatoa mwongozo huo baadaye

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search