Wednesday, 17 May 2017

Mahakama y atoa hukumu ya kesi iliyokuwa inamkabili mkurugenzi wa Halotel na wenzie kuhusu uhujumu uchumi

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Viettel Tanzania ‘Halotel’, Do Manh Hong na wenzake jana walitakiwa kulipa faini ya Tsh milioni 700 baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka saba likiwemo la uhujumu uchumi.
Hukumu hiyo ilitolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam baada upande wa mashtaka kuomba kufanyia marekebisho hati ya mashtaka kwa kuondoa mashtaka matatu kati ya kumi yaliyokuwa yakiwakabili watuhumiwa hao.
Mashtaka mapya ni pamoja na kusimika mitambo ya mawasiliano bila kibali cha TCRA, kutumia mitambo ambayo haijathibitishwa na kuitia serikali na TCRA hasara ya Tsh milioni 459.
Akisoma Hukumu hiyo, Hakimu Wilbard Mashauri amesema amewatia hatiani washtakiwa mwenyewe baada ya kukiri kutenda makosa hayo.
Kabla ya kuwasomea hukumu, Hakimu aliwauliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote ambapo wakili, Johavenes Zacharias ameiomba mahakama kutoka adhabu stahiki kwa washtakiwa.
Naye Wakili wa utetezi, aliiomba mahakama kuwapa adhabu ndogo washtakiwa kwa kuwa hilo ni kosa lao la kwanza na wanafamilia zinazowategemea.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mashauri amewahukumu washtakiwa kulipa faini ya jumla ya milioni 700

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search