Friday, 26 May 2017

MAJERUHI WAWILI WA SHULE YA LUCKY VINCENT WARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALINI

Dar es Salaam. Watoto wawili majeruhi wa ajali ya gari la Shule ya Lucky Vincent wameruhusiwa kutoka hopitalini.

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa watoto hao, Sadia Ismael na Wilson Tarimo waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Mercy ya Marekani wameruhusiwa na sasa wapo katika makazi mapya.

“Watoto Sadia na Wilson waruhusiwa rasmi kutoka hospitali ya Mercy  na wanaelekea kwenye makazi yao mapya mjini Sioux City IA. Mungu azidi kuwaangazia nuru ya uso wake. Amani iwe nawe na Nesi wetu mpendwa kwa huduma kubwa mmefanya kwa watoto hawa na Tanzania,”ameandika Nyalandu.

Jana Nyalandu aliandika kuwa mtoto Doreen ataendelea kuwepo hospitali katika wodi ya watoto akiendelea kupata huduma za karibu hadi itakapoamuliwa vinginevyo

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search