Thursday, 11 May 2017

MASWALI MAGUMU KUTOKANA NA WALIOCHAGULIWA BUNGE LA EALA KUTOKA CHADEMA

Uchaguzi Wabunge EALA!
Viti viwili vilivyobaki kujazwa na Wabunge toka chadema kwenye Bunge la Africa Mashariki, leo limepata baada wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania kuchagua.
Jumla ya Wabunge ni 394, 
Wabunge waliopiga kura ni 296,
Kura halali ni zote 296,
Matokeo;
 Prof Safari 35
Ezekiel Wenje 34
Josephine Ole 219
Lawrence Masha 44
Pamela Masaay 200
Salum Mwalim 54
Niwapongeze Wabunge wote waliochaguliwa na kuwaomba waweke utaifa mbele.
Uchaguzi huu umetuacha na maswali baadhi ya sisi tuliokuwa tukifuatilia, zaidi tukiwa na maslahi ya Taifa kwanza.
 Uchaguzi uliopita ulishindwa kutupatia wawakilisha hao wawili baada ya wagombea wawili walioletwa na Chadema ambao walikuwa Lau Masha na Ezekiel Wenje kupata kura nyingi za hapana na hivyo kulazimisha chadema kupeleka majina 6 ili yapigiwe kura wapatikane hao wawili.
 Zilitolewa sababu nyingi toka kwa Wabunge wa chama Chenye idadi kubwa ya Wabunge kuhusiana na kwanini waliwakataa Masha na Wenje.......
Waliwakataa Wenje na Masha kwamba ni wanaume watupu!
Wameishia kuchagua wanawake watupu!
Walidai, hao wote wametokea Mwanza!
Wameishia kuchagua wote waliotokea Arusha!
Walidai hakuna Mzanzibar!
 Wameishia kumpa Mzanzibar kura ndogo kuliko idadi ya wazanzibar iliyopo Bungeni!
Walidai wagombea wote dini moja!
 Wameishia kuchagua wote wa dini moja!
Nimetafakari sababu za kwanini walikataliwa wagombea wa mwanzo na walivyochagua leo, nikashindwa kuelewa kabisa lengo la Wabunge walio wengi ilikuwa ni nini hasa?
Baada ya kukumbuka sifa za vyeo vya kisiasa yaani KKK, nikaamua nisichanganyikiwe zaidi!
Leo Spika anasema wananchi wanataka kushuhudia live kila hatua uchaguzi inavyokwenda ili wajue wagombea wote na jinsi watakavyochaguliwa!
Lakini Spika huyohuyo, bado hajaona umuhimu wa wananchi kuona na kufuatilia vikao vya Bunge live hasa kipindi hiki muhimu cha Bajeti ili waelewe bajeti yao Wizara kwa Wizara hadi Bajeti kuu na kuwashauri wabunge wao waliowachagua nini wanataka waongee kuboresha bajeti. Hilo kwa Wabunge walio wengi pamoja na Spika hawajaliona!
Tukiendelea na sifa ya KKK, nchi yetu itatuchukua muda mrefu sana kufika tunapopataka maana hawa wanasiasa ndio viongozi wetu.
Sio kwamba napingana na KKK, naelewa wengine KKK lakini busara zao ni zaidi ya PhD, ninaongelea kwa kuoanisha na matukio yanayoendelea kwasasa

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search