Tuesday, 9 May 2017

MKAPA;KWANINI SIKUFANYA UHAKIKI WA VYETI WAKATI NIKIWA MADARAKANI


BAADA ya Rais John Magufuli Kubaini watumishi wenye vyeti feki kwenye Serikali na kuwatoa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjami Mkapa amejialumu kwanini hakuafkilia kuhakikia vyeti feki kwa watumishi wa umma alipokuwa madarakani

“Masikitiko yangu pekee ni kwamba kwa nini sikufanya uhakiki huu wakati nikiwa madarakani. Labda nilikuwa na mambo mengine makubwa zaidi niliyotakiwa kuyafanya lakini kwa hili alilofanya Magufuli namuunga mkono kabisa,” alisema Mkapa.

Kauli hiyo ameitoa alipokuwa akifanya mahojiano na Shirika la Habari la Ujerumani (DW)  na Kumpongeza rais Magufuli  kwa kufanikisha zoezi la kuondoa wafanyakazi hewa na wenye vyeti vya kughushi vya taaluma na kazi, na akasema anasikitika tu kwamba kwa nini yeye hakufanya hivyo wakati wa utawala wake.

''Wenye vyeti feki au watumishi hewa walikuwa wakiingizia serikali hasara wengine wakiendelea kukaa kazini bila ya kustaafu, hivyo lilikuwa ni jambo la lazima kufanyika ni kwa manufaa ya taifa" amesema


Kauli hii ya Rais Mkapa imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Rais Dkt Magufuli kuwaamuru watumishi wa umma 9,932 waondoke kwenye utumishi wao baada ya kubainika kughushi vyati vyao

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search