Wednesday, 10 May 2017

MKURUGENZI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUSHINDWA KUFANYA MALIPO KWA KUTUMIA RISITI ZA EFD

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Hotel ya Break Point, David Machumu amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni akituhumiwa kwa mashtaka matatu likiwemo la kushindwa kutoa risiti katika mashine za elektroniki (EFDs).

Akisoma  hati ya mashtaka  Wakili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) wa  Wilaya ya Kinondoni, Juliana Ezekiel amedai kuwa  tukio hilo lilitokea Oktoba 8, mwaka 2016 katika hoteli hiyo iliyopo Kinondoni.

Wakili Ezekiel amedai kuwa mtuhumiwa kwa makusudi na bila sababu alipokea Sh12,000 kutoka kwa mteja ajili ya vinywaji bila ya kutumia mashine za EFDs ambapo kufanya hivyo ni kosa kinyume cha sheria ya kodi.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search