Thursday, 4 May 2017

MUBASHARA PROFESA LIPUMBA ANAONGEA NDANI YA KIPINDI CHA CLOUDS 360 AKIELEZEA MAMBO MBALIMBALI NDANI YA CUFProfesa Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa leo anaongea katika kipindi maarufu cha Clouds TV cha 360.

Ni suala la msingi kama Katibu mkuu angeheshimu katiba ya Chama hakuna tatizo, Katibu Mkuu anajiona ni Sultan hashauriki.

Mfano upo wazi Mimi nilijiuzulu wakati yeye bado hajaitisha Mkutano mkuu mimi nilitengua uamuzi wangu.

Nilijiuzulu tarehe 5 Agosti 2015 sababu kutokuwepo kwa Umoja ndani ya chama na Makatibu wakuu wa UKAWA.

CHADEMA walitumia nafasi kutugawa sisi wakisema hatuna mpango na Rasilimali fedha kumsimamisha mgombea Urais.

Nilikuwa sina nia ya kurudi kilichonifanya nirudi ni hali ya uchaguzi wa Zanzibar kuirudisha CUF katika Umoja.

Baada ya kuzungumza na Wananchi kuhusu hali ya Zanzibar kama mwanachama Maalim Seif aliniandikia barua pepe na kunipongeza.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu walifika nyumbani kuniomba nirudi nafasi ya uenyekiti walikuwa wanasema Maalim hana tatizo na mimi.

Mimi nilitaka kugombea pia Dr Kuhangwa alitaka kugombea tulikubaliana kumuunga mkono Dr Slaa ambaye alikuwa na nguvu zaidi.

Mimi nilijiuzulu kweli hili tatizo si la kikatiba nilipitishwa na Mkutano mkuu Maalim Seif aliniomba nisubiri kwanza.

Siyo mimi niliyetaka hii nafasi ni wanachama waliniomba kurudi kutetea hali ya Chama chetu.

Nilimfuata Maalim Ilala kumueleza kwanini nilijiuzulu na kwanini nilirudi ndani ya CUF akasema atalipeleka kwenye vikao.

Walipoitisha Mkutano Mkuu pale Blue Pearl sikupewa nafasi ya kujieleza nikishangaa kura 476 zinanikataa 14 zinataka nirudi.

Baada ya matokeo yale pale Blue Pearl Ubungo wajumbe wakaanza kuimba bora Jecha kuliko Maalim Seif.

Mwaka 2000 baada ya Uchaguzi tuliingia kwenye maandamano Zanzibar Maalim Seif alikwenda Uingereza nilikuwa mstari wa mbele.

Mbatia ndiye aliyeniunganisha na Lowassa sikuwa na namba zake na wakati anakuja nilisema wazi suala la Rushwa ni mfumo siyo mtu.

Ninachomlaumu Maalim Seif ni kutokutoa ushirikiano ndani ya chama chetu cha CUF, Chadema walituzidi kete.

Waliotusaliti ni wale waliomleta Edward Lowassa ndani ya UKAWA siyo sisi ambao tulijitoa ndani ya vyama vyetu.

Katiba ya Chama cha CUF haitambui kamati ya Uongozi iliyopo ni kinyume cha kifungu cha 8 katika katiba yetu.

Mimi sipokei ruzuku ya Chama tulipokea mara moja tu, sikuvamia ofisi za Chama bali msajili aliponitambua nilikwenda pale.

Vijana wetu wa Blue Guard ambao Maalim anawaita Maharamia ni sehemu ambayo yeye aliwasainisha mwenyewe vitambulisho.

Mimi bado ni mwenyekiti wa CUF na Maalim ni Katibu Mkuu ila tatizo hafiki ofisini nimpangie majukumu yake!

Maalim Seif anatumia ubabe kuwadhibiti Wabunge ambao wananiunga mkono wapo Wabunge 42 wenye msimamo ni wawili tu.

Mimi niliwahi kuwa CCM lakini sikuwahi kuwa kindakindaki nilikuwa mwanachama wa kawaida tu.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search