Tuesday, 30 May 2017

MWANAMKE- FANYA HIVI ILI MUMEO AKUBALI KWA URAHISI UNACHOKITAKA

1.    Mwambie mumeo unachokitaka pindi anapokuwa ametulia ambapo hana msongo wala mizigo ya mambo. Ukiandaa kitu kinachoitwa USIKU WA MUME itakuwa vizuri zaidi na hapo unaweza kumwambia jambo lako.

2.    Ikiwa jambo husika sio la dharura usimwambie kwenye simu, bali msubiri atakapokuja akakaa na kupumzika.

3.    Anapotoka kazini usimwambie ghafla mahitaji yako, kwa sababu huo ndio muda ambao anajaribu kuondokana na mizigo na mashinikizo ya kazini.

4.    Wafundishe watoto wako muda muafaka wa kumwambia baba yao mahitaji yao kwa sababu muda ndio kichocheo kikubwa cha msongo wa mwanadamu

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search