Friday, 26 May 2017

MWANAMUZIKI BEN POL AZUNGUMZIA PICHA YAKE YA UTUPU

Kwa siku za hii karibuni mwanamuziki wa miondoko ya RnB , Benard Paul maarufu kama Ben Pol amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii kufuatia kuchapisha picha inayomuonyesha akiwa utupu.
Ben Pol alichapisha picha hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram inayomuonyesha akiwa amekaa kwenye kiti mtupu huku mikono yake ikiwa imefungwa nyuma ya kiti. Baada ya kuchapisha picha hiyo, hakuandika maelezo yoyote huku washabiki wake na watu wengine wengi wakionyesha kuchukuzwa na picha ile.

A post shared by BEN POL (@iambenpol) on 
Mbali na mashabiki wake waliyotoa maoni yao, wasanii wenzake pia wameonyesha kutoelewa Ben Pol amemaanisha ni i kwa kuchapisha picha ya namna ile kwani wengi walimchukulia kama mtu mstaarabu asiye na mambo ya hivyo.
Akizungumzia picha hiyo mwanamuziki Kala Jeremiah alisema yeye anaamini kwamba watu wamedukua akaunti ya Ben Pol na kuedit picha yake, hivyo haamini kama ni Ben Pol mwenye amechapisha picha ile.
“Nilivyoona picha mimi nilihisi hivyo kwa akaunti yake imehakiwa kisha wale watu waka’edit’ picha zake. Siamini kama ni Ben Pol, Ben Pol mimi namfahamu kitambo sana, nimefanya naye ngoma, ni mtu ambaye anajielewa sana na anajiheshimu” alisema Kala.
Kwa upande wake Shilole, alisema yeye hajaelewa sababu ya Ben Pol kupiga picha ile na kwamba asingependa kuhukumu pasi na kujua sababu iliyopelekea hatua hiyo.
Shilole alisema tukio kama lile kutokea kwa mwanaume ni la kushangaza, hasa kwa mtu kama Ben Pol kwani waliozoeleka kupiga picha za utupu ni wanawake.
Licha ya hayo yote kuzungumzwa na watu mbalimbalia, mhusika mkuu wa tukio hilo, Ben Pol amewataka watu kutokuhumu jambo wasilolijua kabla hayajaelewa lengo kuu.
Kupitia chapisho la mwisho aliloliweka kwenye ukurasa wake, ambalo aliambatanisha na wimbo unaosikika ukiimbwa, Ben Pol aliandika, “Usi-judge kitabu kama hujakisoma ndani 🤔

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search