Thursday, 4 May 2017

MWANAUME-ZIFAHAMU SIFA ZA MWANAMKE ANAYEFAA KUOLEWA

Image may contain: one or more people, people standing, shoes and outdoor
Binti zingatia haya ili uolewe, wanaume wamebaki wachache n wanawake kila siku wanaongezeka_fact.
Katika siku hizi za kisasa za sayansi na teknolijia wanaume wengi wamejikuta katika mkanganyiko mkubwa hasa linapokuja suala la kutafta mchumba au mwenza wa kumuoa na kuanzisha maisha na familia. Kijana wa kiume unaweza kutembea na msusruru wanawake ila linapokuja suala la kuoa basi lazima kidogo utilize kichwa kwa kuwa ndoa si lelemama na ni mkabata ambao hauvunjwi kirahis.
Leo nimekulea hapa baadhi tu ya sifa za masingi ambazo mwanamke anatakiwa awe nazo kama unataka kuoa. Pia km mwanakmke unataka kuolewa na kuishi na mme zisome hizi sifa naamini zitakusaidia sana:.
1: Tabia njema: uzuri wa mwnamke ni tabia mimi naamini hivo ndio maana hata mwanaume atadate na wanawake wazuri ila akitaka kuoa lazima aangalie yupi ana adabu na tabia njema moyoni mwake. Si maanishi wazuri hawaolewi ila kuwa na tabia njema ni kigezo kikubwa cha mwanamke kuolewa so jitahidi kutengeneza tabia yako ikawa ya staha kwa mwanaume…
2: Anyeshika dini, kuna wanawake wengi wazuri sana ila hawashiki dini. Tunaamini kuwa anayaeshika dini huwa na heshima kwa mumewe kwa kuwa hata dini inafundisha hivo. Japo si wote wanaoshika dini huwa na heshima ila aghalabu wale waliosalia katika dini huwa na hashima sana kwa waume zao. Pia ni rahisi mtuhuyu kuwafundisha watoto njia njema na salam ktika ulimwengu huu wa kisasa
3: Heshima na adabu, hapa hekima inahitajika kujua yupi anaheshima, unakuta mwanamke ni mzuri ila hana hata chembe ya heshima, ni kuropoka hata mavazui yake si ya heshima, sijui nguo zimechanika chaninka au nguo za kulalia anavaa mchana na za machana usiku. Kama anshindwa kuwa na heshima hata juu ya mwili wake atakuheshimu wewe mwanaume? So badilika dada yangu ili usiseme ulizaliwa na mikosi huolewi kube unajitakia tu.
4: Anaye vaa kwa staha na heshima, mwanamke avae kwa staha sio anavaa kama mhuni au kahaba Fulani hivi. Mwanamke usivae tu kisa fasheni au kwa kuwa fulani kavaa, au ili uoneshe kuwa una kiuno na vitu km hivyo. Unavaa nguo mpaka ukipita kwa watu unajistukia? Aibu na ndio nguo hizo zinafanya wanaume watamani na wengine wanaweza kujua ni mhuni kupitia tu nguo ulizo vaa hata kama si tabia yako. Usiseme waendana na wakati, nguo gani ambazo hazikupi uhuru ukitembea. Mwanaume unamnunulia mchumba vinguo vya ajabu akivaa wanamtamani wanamtongoza-na hawezi kukataa wanamla, usilalamike chanzo ni wewe. Suala la maadili ni muhimu mno ktk mavazi, SIKUHIZI MWANAMKE AKIVAA STARA ATAITWA MSHAMBA NA AMEPITWA NA WAKATI ,,, LAKINI AKIVAA NUSU UCHI ATAITWA MTOTO MKALIIII mimi siamini kama ili uonekane mrembo zaidi ni lazima uvae nusu uchi.... Wakati huohuo asilimia kubwa ya wanawake walio olewa ni wale wanaojisitiri vema!!!!! Jamani tumuogopeni mwenyezi Mungu
5: Anayependa na kuwaheshimu wazazi, ni wajibu wa mwanamke kuwapenda wazazi wake na wa upande wa kiume. Unadate na binti unakuta hata wazazii wake hawapendi na hata wakwako hawapendi wala kuwa heshimu, huyo ni jipu muache kwani ipo siku mama atakuja kukutembelea badala ya kupikiwa atamgeuza mamamkwe housegirl. Acheni heshima za kinafiki.
6: awe na mapenzi ya dhati na anayejua kupenda, wengi wameumi sana kwa kupenda au kupenda kisa mtu anakitu Fulani aidha fedha au mali. Kumbuka furaha na upendo wa kweli hautokani na mali au pesa, mwamke asikupendea kwa kuwa una pesa au wewe ni meneja, ukifirisika lazima uone dunia kama kuzimu vile. Ewe binti usimpende mtu sababu ya pesa au uatajiri kwani hivi vitu vinapita, jali utu na thamni ya mtu si mali au cheo chake. Kuna watu wnapesa ila ndoa zao ni machungu mnoo..bora maskini anayepata upendo kuliko tajiri mwenye machungu ya moyo.
7: Kauli njema na za adabu, chunguza kauli zake je za kutia moyo au kukatisha tamaa? Yaani awe mtu wa kukutia moyo wewe mwanaume, anakuongelesha kwa heshima sio anakuwa mkali kama askari wa zamu wa jeshii la zimamoto. Ndio maana mwanaume alioa akiwa bonge gafla anaconda na kuwa kma mbu wa kiangazi, kauli zinafanya wanaume wanakimbia uhusiano, utasikia naenda kwa Jeni rafiki yako, yes ataenda kwa kuwa wewe hujui kuongea na mpenzi wako vizuri. Binti ichunge kila kauli uitoaye pindi uwapo na boyfriend au mchumba wako.
8: Mwenye malengo na mtazamo wa kimaendeleo, siku hizi wnawake wameamka sana wanapenda kuendeleo, awe mtu mwenye mipango ya mbele ya namna ya kuendesha familia na kufanikiwa, awe anashirikiana nawe katika kutekeleza miapngo ya maendeleo na si kung’ang’ania nywele na mawigi ya elfu 70 wakati mnaishi nyumba ya kupanga, huyo mwogope kama ukoma.
9: Asiwe mtu wa makundi sana na starehe, ktk vitu vinavyofanya mwanamke akakosa adabu ni makundi. hatukatai kila mtu anazungukwa na watu ila makundi mengine yanabomoa, utasikia “we mjinga mwanaume mmoja pekee atakusaidia nini”. Kuwa makini na makundi ambayo mchumba au boy/girlfriend anaishi nayo. Kuna wanawake vichwa vyao vyawaza kubomoa uhusiano wa wengine, wanawaza pombe, mziki, starehe na kulewa, hayo makundi yaogope kama ukoma.
10: Asiyependa kuiga, utasikia “beby nataka simu kama ya Mwajuma ile Iphone 7” au si jui gauni la Angel. unajua boyfriend wako hana uwezo ila unaiga kwakuwa fulani anayo, huo ni ujinga. Mwanaume muepuke mara moja binti kama huyu kwani ipo siku utashindwa kumnunulia na atakuacha. Mwanamke bora haigi kila kitu…
11. Asojivunia uzuri wake, mwanaume unakutana binti kauli zake tu ni kukutishia eti mzuri mi sana! Mimi nasemaga hata Cleopatra alikuwa mzuri ila alimtii mumewe, wewe nani hata ujidai na uzuri wako? Uzuri huo ni nini? Eti nina kiuno! Sio kweli kabisa, Ndio maana kuna mwanasaikolijia alisema mwanaume ukitaka kuishi kwa stress “oa mzuri sana” simaanishi usiwe na mwanamke mzuri ila asiwe wa kujivunia uzuri wake. Waswahili wana sema “kama Mzuri Olewa” so usipende sana kutumia uzuri kama silaha okay…
12: Anasikiliza na kukutii, mwanamke bora huwa anakuwa msikilizaji, anahoji vizuri na kwa utulivu, sasa unakuta mtu ni mchumba tu hata hujamaliza ulicholikuwa unaongea kasha dakia, majibu ya ovyoovyo, hiyo ndoa lazima iwe ya kibondia na kwa wenye miili midogo kama yangu utakonda bure ufe uache wazazi na watoto...
13: Usafi, kiufupi wanawake wameumbwa na hulka ya usafi, awe mtu wa kupangilia vitu vizuri anavaa kwa unadhifu kiasi hata ukitembea nae njiani huogopi kumtambulisha. Usafi huu ni wa ndani na nje, kumbuka mwili wa mwanamke ni tofauti na wa kiume, km hapendi usafi saa hizi na hamna watoto itakuwaje majukumu yakiongezeka? Ndio pale unampeleka rafiki yako kwako na kukutana na viatu juu ya meza….
14: Asiwe mtu wa ugomvi, tuanaamini kuwa mwanamke aliumbwa mpole na mnyeynyekevu, awe angalau mtu wa kushuka hata ukimkosea, ili kwa kinywa chake asiharibu ndoa na uhusiano. Unakuta mwanamke mgovi kitu kidogo tu maneno mengi mpaka mtaa wa tatu wanasikia. Hapa mwanamke ujue una lazimisha mwanaume atafute kimada anayejua kutuliza kinywa chake!
15: Mchapa kazi, simaanishi awe ameajiriwa au awe na kazi ila namanisha anayewza kutimiza majukumu yake vizuri na kwa wakati. Sio unamnunulia mboga mapema, unarudi kazini unakutahata vyombo vya jana hajaosha na kupika hajapika. Mwanamke usiwe mtu wa kupangiwa majukumu jiongeze, ukiona nguo chafu fua, usisubiri kuambiwa. Ukitekeleza majukumu vizuri lazima upendwe tu…

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search