Thursday, 18 May 2017

MWENYEKITI WA CCM TAWI LA NJIA NNE AUAWA KWA KUPIGWA RISASI WILAYANI KIBITI


Mwenyekiti wa CCM tawi la Njia nne Iddy Kirungi liliopo katika kijiji cha Muyuyu kata ya Mtunda wilayani  Kibiti ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa kwake.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Juma Njwayo,ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji amethibitisha kutokea mauaji hayo.

Amesema marehemu alipigwa risasi akiwa kwake wakati akijaribu kukimbia.

Njwayo amesema kabla ya kuuawa kwa mwenyekiti huyo, pia wauaji hao walianza kumjeruhi kwa kumpiga risasi ya tumboni mtoto wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Nurdin Iddy Kirungi.

Mganga wa zamu katika kituo cha afya Ikwiriri, Dk Rashid Omar alisema walimpokea Nurdin akiwa na jeraha kubwa tumboni mwake ambalo halikutokeza upande wa pili.

Alisema majeruhi huyo walimpatia rufaa kwenda Hospital ya Mchukwi kutokana na kuwa anavuja damu nyingi sana

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search