Monday, 29 May 2017

NGULI WA SOKA FRANCESCO TOTTI ATUNDIKA DALUGA BAADA YA MIAKA 25 AKIWA NA ROMA

Nguli wa soka Francesco Totti amehitimisha miaka yake 25 ya kusakata soka akiichezea Roma mara 786 na kwa mara ya mwisho jana wakishinda magoli 3-2 dhini ya Genoa katika mchezo wa mwisho wa ligi ya Serie A katika msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40, aliingia dimbani katika dakika ya 54 akitokea benchi, na sasa anatarajiwa kuwa Mkurugenzi wa Roma, ingawa pia kunauvumi kuwa huenda akaenda kusakata soka kwingine.
                               Francesco Totti akinong'onezwa jambo na mkewe Llary Blasi 
     Francesco Totti akiongea kwa kutumia kipaza sauti akiwa na mkewe pamoja na watoto wake

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search