Tuesday, 9 May 2017

PICHA:HIVYO NDIVYO MASHUJAA WETU WALIVYOAGWA MKOANI ARUSHA


ARUSHA: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan amewaongoza mamia ya waombolezaji waliofika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha pamoja na Watanzania wote kuaga miili a watoto waliofariki kwa ajali ya gari juzi Jumamosi.


Akitoa salam za rambirambi kwa wafiwa na Watanzania wote, Bi Samia amewataka walioguswa na msiba huu kuwa wavumilivu na kumtegemea Mungu hasa katika wakati huu mgumu kwa Taifa.
Aidha Bi Samia amemshukuru Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Wakenya kwa ujumla kwa kuungana na Wananchi wa Tanzania katika msiba uliotokea.
Katika ajali hiyo iliyotokea Wilayani Karatu juzi Jumamosi, baada ya basi aina ya coaster lililokuwa limebeba wanafunzi wa Lucky Vincent Primary School wakielekea kwenye mtihani wa kujipima na wenzao kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo, jumla ya watu 35 wameaga dunia wakiwa ni wanafunzi 32, walimu 2 na dereva mmoja.
Serikali imesema italipia gharama zote za kusafirisha miili 35 ya waliofariki katika ajali ya hiyo ambao ni wanafunzi, walimu na dereva wa Lucky Vicent.
Majeneza yenye miili ya marehemu yakishushwa kwenye gari na kupelekwa sehemu maalum kwa ajili ya kuagwa.
Majeneza yenye miili ya marehemu.
Bi. Samia akiwatia moyo wanafunzi wa Lucky Vincent
Waombolezaji wakilia kwa uchungu.
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiongozana na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakati wa kuaga miili ya marehemu hao.
Sehemu ya waombolezaji.

Waombolezaji wakiwa katika viunga vya Hospitali ya Mount Meru Arusha wakisubilia miili ya watoto hao kwa ajili ya kuagwa.
Bi. Samia akiwa mwenye masikitiko makubwa.
Kikosi cha Huduma ya Kwanza wakitoa msaada kwa waliopoteza fahamu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jinsia na Watoto, Dkt. Ummy Mwalimu akitoa salam za pole kwa wafiwa na Watanzania wote.
Wanafunzi wa Lucky Vincent wakionesha nyuso za hudhuni wakati wa kuaga wenzao 32, walimu wao na derva.

PICHA NA HILALLY DAUDI | GLOBAL PUBLISHERS

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search