Monday, 29 May 2017

POGGA AKIWA MAKKAH KUHIJI

Nyota wa Manchester United, Paul Pogba, amekwea pipa na kutua nchini Saudi Arabia na kushiriki siku ya kwanza ya mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni siku tatu tu kupita tangu abebe kombe la Ligi ya Uropa.

Pogba aliyevalia vazi la kitambaa cheupe akiwa amekata nywele zake kwa mtindo mpya wa nywele fupi alionekana miongoni mwa mahujaji waliokuwa katika mji wa Makka baada ya kuanza mfungu wa Ramadhani siku ya jumamosi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye ni muumini wa dini ya Kiislamu, haijajulikana iwapo atafunga mwezi mzima wa Ramadhani, huku akiwa ameitwa katika kikosi cha kocha Didier Deschamp wakati Ufaransa itakapowavaa Paraguay, Sweden na Uingereza mwezi Juni.
Paul Pogba akionekana amevalia vazi la kitambaa cheupe akiwa pamoja na waumini wengine wa dini ya Kiislam huko Makka
                  Mchezaji nyota wa Manchester United Paul Pogba akipozi kwa ajili ya picha

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search