Thursday, 11 May 2017

Profesa Kabudi awasilisha cheti UDSM

Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi 

Dodoma\ Dar. Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi  amesema tayari amewasilisha cheti cha kidato cha nne katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa ajili ya kupelekwa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) kwa ajili ya uhakiki.

Akizungumza na gazeti hili bungeni mjini hapa jana, Profesa Kabudi alisema cheti hicho alikuwa ameshakiwasilisha kwa uhakiki lakini hajui ilitokea nini hadi ikaonekana hakipo.

Jina la Profesa Kabudi limetokea katika orodha ya watumishi wa UDSM ambao vyeti vyao havikukamilika kwa uhakiki.

“Yaliyotokea huko siyajui na hayanihusu, ila unachoweza kuandika ni kwamba nimeshawasilisha cheti changu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wao watakipeleka kwa Necta kwa uhakiki,” alisema.

Huku akionyesha picha ya cheti hicho kwenye simu, Profesa Kabudi alifafanua kuwa wakati aliposoma yeye haikuwa rahisi kutokuwa na cheti cha kidato cha nne na ukachaguliwa kuingia kidato cha tano kwenye shule za umma.

Mawakili kadhaa wamemtetea Profesa Kabudi  kwamba kutajwa kuwa na matatizo kwenye vyeti vyake imetokana na mfumo mbaya unaotumika na Serikali katika uhakiki.

Wakizungumza na Mwananchi jana  kwa nyakati tofauti wameeleza kuwa utekelezaji wa uhakiki wa vyeti ni hatua muhimu na yenye maana kwa maendeleo ya Taifa lakini umefanywa katika mazingira ambayo si makini kiasi cha kudhalilisha watu wenye hadhi zao katika jamii.

Wakili Alex Mgongolwa alisema uhakiki huo ungefanywa na Serikali kwa kuwasiliana na vyuo au taasisi husika ili kupata majibu ya uhakika, kuliko kuwaamuru watumishi wawasilishe vyeti

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search