Friday, 26 May 2017

RAIS MUGABE AMTEUA MWANAE KUSHIKA WADHIFA SERIKALINI

Binti wa kipekee wa rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Bona Mugabe-Chikore, ameteuliwa katika bodi ya udhibiti vyombo vya habari na sekta ya filamu nchini katika kile ambacho wakosoaji wanasema ni hatua ya kusaka taarifa zinazoipinga familia hiyo, hususan katika mitandao ya kijamii.
Msemaji wa Polisi Charity Charamba pia atahudumu katika bodi hiyo ya watu 11 iliyoteuliwa na waziri wa mambo ya ndani Ignatious Chombo, pamoja na wawakilishi wa makundi ya makanisa, wataalamu wa sheria na uhasibu na vioongozi wa kitamaduni, anaarifu mwandishiw a BBC kutoka mji mkuu, Harare.
Shirika la kitaifa la habari imesema bodi hiyo itadhibiti na kukagua vyombo vya habari na sekta ya filamu nchini na kulenga “matumivi mabaya ya mitandao ya kijamii wakati pia ikizingatia uchaguzi mkuu unaowadia mwaka ujao”.
Bi Mugabe-Chikore amesomea Singapore, na ana shahada ya uzamili katika masuala ya usimamizi, hususan wa mabenki na fedha.
-bbcswahili

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search