Tuesday, 30 May 2017

ROFESA MUHONGO AZUNGUMZA KWA MARA YA KWANZA JIMBONI KWAKE TANGU ATUMBULIWE

Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Musoma Vijiji Prof. Sospeter Muhongo amewasihi wakazi wa jimbo hilo kutokuingiwa na hofu kufuatia uamuzi wa Rais Dkt Magufuli kumfuta kazi.
Prof. Muhongo amewataka wapigakura wake na rafiki zake kutokuwa na hofu kwani kwa pamoja watafanikiwa.
Kwa mujibu wa taarifa za ofisi yake, amewaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha kuwa wanafikia malengo yao ya kimaendeleo kwa kutimiza ahadi zake.
Taarifa hiyo ilitolewa na Katibu wa Mbunge huyo, Juma Ramadhan ambaye alisema kuwa kilichotokea ni cha kawaida kwenye siasa na inawapasa kusahau hayo ili waweze kusonga mbele katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
Kwa sasa tunajielekeza kujenga vyumba vya madarasa na miradi mingine ya maendeleo, hivyo ni vyema tukaungana pamoja ili kuweza kutekeleza majukumu haya, alisema msaidizi huo.
Wakazi wa jimbo hilo waliahidi kutoa ushirikiano kwa mbunge wao katika kutekeleza miradi hiyo kwani yeye si kiongozi wa kwanza kuondolewa kwenye wadhifa wake. Aidha, wakazi hao walisema kuwa kuondolewa kwa Prof. Muhongo kuwe funzo kwa wateule wengine kuwa nafasi hizo si za kudumu.
Mei 24 mwaka huu Rais Dkt Magufuli alimfuta kazi Waziri Muhongo kufuatia kile alichosema ni kushindwa kusimamia kwa umakini sekta ya madini na hivyo kupelekea serikali kupata hasara.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search