Monday, 15 May 2017

SHIRIKA LA AFYA DUNIANI KUPAMBANA NA EBOLA NCHINI DRC

Shirika la Afya Duniani, WHO limeahidi kuchukua hatua za tahadhari na za haraka, ili kuzima mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola uliotokea kaskazini mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
WHO Imesema kuwa wataalamu wake wa kiufundi, wametumwa hadi maeneo ya vijijini, kunakoaminika kutokea visa 11 vya ugonjwa wa Ebola, zikiwemo ripoti ya vifo vya watu watatu.
Wanafanya kila mbinu kubaini kasi ya mlipuko wa ugonjwa huo, kuwapa tiba walioambukizwa na virusi vya ugonjwa huo, na kuwatambua walioambukizwa au watu waliokaribiana na walioambukizwa virusi hivyo.
Huu ni mlipuko wa 8 uliotambuliwa wa Ebola nchini Congo, tangu kisa cha kwanza kutambuliwa cha Ebola nchini humo mnamo mwaka wa 1976

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search