Wednesday, 10 May 2017

UMESIKIA HAYA YA MSUKUMA-AWAUMBUA WABUNGE ADAI WOTE WALIENDA KWA WAGANGA WA KIENYEJI 2015 KASORO WAWILI LAKINI LEO WAMEWASAHAU

Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma (ambaye ni mwakilishi wa waganga wa kienyeji Bungeni amesema karibia wabunge wote waliopo bungeni isipokuwa wabunge wawili tu ndiyo hawakupita kwa waganga wa kienyeji kipindi cha uchaguzi Mkuu 2015.

Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Msukuma akihotubia katika moja ya mkutano wake kipindi cha kampeni za Uchaguzi 2015.

Msukuma amedai kuwa wabunge hao baada ya kupita katika chaguzi zao wamekuwa wakiwasahau waganga hao wa kienyeji na kufikia hatua ya kuwatumia polisi ili wawakamate badala ya kuwasaidia, hivyo Mbunge huyo ameiomba serikali japo kuwajengea hata chuo tu waganga hao wa kienyeji kwa kuwa wamekuwa wakifanya mambo mengi yanayosaidia katika jamii.

"Nimekuwa nikisikia wabunge wakiwatetea sana wasanii humu ndani wanawasahau waganga wa kienyeji. Kwa karama niliyonayo nikiwaangalia Wabunge humu ndani wakati wa uchaguzi wote hakuna ambaye hakupita kwa waganga wa kienyeji, labda wawili ambao hawakupita kwa waganga akiwepo Mh. Joseph Selasini lakini Mh. Spika siyo wabunge tu pekee yao hata jamii nzima, lakini cha ajabu waganga hawa baada ya Uchaguzi tunawatelekeza na kuwaitia polisi" alisema Msukuma

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search