Friday, 26 May 2017

VIDEO: MCHUNGAJI ADAI KUZUNGUMZA NA MUNGU KWA NJIA YA SIMU

ZIMBABWE: Ki ukweli nina namba ya simu ya mbiguni ambayo naweza kupiga simu na kupata maelekezo moja kwa moja kutoka kwa Mungu kuhusu namna ya kuwasaidia watumishi wake, alinukuliwa akisema.
Mchungaji Paul Sanyangore kutoka Victory World International Ministries amzeua gumzo baada ya video yake akiwa mbele ya umati wa waumini akidai kuwa ana namba ya simu ya mbinguni kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Katika video hiyo iliyowashangaza wengi, mchungaji huyo anaonekana akimuombea mwanamke mmoja na ghafla anaanza kuongea na simu kwa kile alichodai kwamba anapokea maagizo kutoka mbinguni.
“Hello, hapo ni mbinguni? kuna mwanamke hapa, una nini cha kusema kuhusu yeye? Oh.. nimuulize Sibo ni nani,” anaonekana mchungaji huyo akizungumza kwenye simu.
Video hiyo inaenda mbele zaidi ikionyesha mchungaji akiendelea na kile alichodai ni kuzungumza na Mungu na kumueleza mwanamke huyo maagizo aliyopewa na anayedai kuwa ni Mungu.
Mwanzoni mwa mwezi huu mchungaji huyo aliahidi kuziweka hadharani namba hizo za simu anazotumia, lakini hadi sasa bado hajafanya hivyo. Licha ya kuwa video hii ilirekodiwa mwezi Machi mwaka huu, lakini siku ya leo ndio imekuwa ikijadiliwa zaidi mitandaoni nchini Zimbabwe na Afrika Kusini.
Tazama video hapa chini;Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search