Tuesday, 9 May 2017

Zitto: Nimeomba mkataba rasmi wa ununuzi wa ndege

Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuna matatizo makubwa katika manunuzi ya ndege aina ya Boeing jambo ambalo limepelekea Mbunge huyo kuomba mkataba wa ndege hiyo bungeni

Zitto Kabwe amesema hayo baada ya gazeti la Jamhuri kuandika taarifa juu ya ndege hiyo huku likisema kuwa Zitto Kabwe ameshindwa na kudai anapotosha Umma juu ya taarifa za ndege hiyo, jambo ambalo Zitto Kabwe analipinga vikali na kusema gazeti hilo linatumika na watu wanaohangaika kuficha ukweli juu ya manunuzi ya ndege hiyo na kusema watake wasitake watajibu tu ukweli.

"Nimeomba mkataba wa ndege hii rasmi Bungeni. Nitawapa mrejesho. Kuna tatizo kubwa kwenye manunuzi haya. Boeing Airplanes wamepaniki sana na wanunuzi, wamekazana kuficha ukweli kuhusu ununuzi wa Ndege hii. Watajibiwa tu, aste aste" alisema Zitto Kabwe
Nimeomba mkataba wa ndege Hii rasmi Bungeni. Nitawapa mrejesho. Kuna tatizo kubwa kwenye manunuzi haya. @BoeingAirplanes wamepaniki Sana https://twitter.com/zittokabwe/status/861810631648960512 

Gazeti la Ikulu hili kaka. Wanahaha wao na @BoeingAirplanes kuficha ukweli kuhusu ununuzi wa Ndege Hii. Watajibiwa tu. Aste Aste https://twitter.com/gtelemka/status/861803996696203264 


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search