Wednesday, 28 June 2017

Breaking News: KIBITI: Mtendaji wa Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi wauawa kwa kupigwa risasi

Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi katika kijiji cha Mangwi kilichopo Kata ya Mchukwi wilayani Kibiti usiku wa kuamkia leo (Jumatano).

Waliouawa wametajwa kuwa ni Mtendaji wa kijiji hicho, Shamte Makawa na mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Maiko Nicholaus.

Habari za awali zinaeleza maiti ya mwenyekiti huyo wa kitongoji bado haijaonekana na nyumba zao zimechomwa moto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amekiri kutokea kwa mauaji hayo.

Amesema polisi wameenda eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji na ukaguzi.

Watu 37 wameuawa kwa kupigwa risasi tangu vitendo vya mauaji vilipoanza katika wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani Januari 2015 wakiwamo askari 13 wa polisi.


Chanzo: Mwananch

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search