Friday, 9 June 2017

BREAKING NEWS:KIBITI: Watu wengine watatu wauawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo

Pwani. Habari zilizotufikia hivi punde zimeeleza kuwa watu watatu wakazi wa kijiji cha Nyamisati, wilayani Kibiti wanadaiwa kufariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.

Mkazi mmoja wa Kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina moja la Hamza amesema miongoni mwa watu waliopigwa yumo mwanamke mmoja ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji kimojawapo kijijini hapo.

Wanaosadikiwa kupoteza maisha ni Hamid Kidevu,Yahaya Makame na Moshi Machela.

Mkuu wa wilaya ya Kibiti Gullamuhusein Kifu amesema ameliagiza jeshi la Polisi wilayani hapa kwenda eneo hilo kwa ajili ya uthibitisho.

Tutaendelea kukuletea habari zaidi kuhusu tukio hili.

Credit: Mwananchi

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search