Tuesday, 20 June 2017

IMETOLEWA RUKSA KUKOSOA SERIKALI


Mkurugenzi wa Habari Maelezo Dkt. Hassan Abbasi amefunguka na kusema hakuna chombo cha habari ambacho kitachukuliwa hatua na serikali kwa kuandika habari zenye mrengo wa kukosoa sera na utekelezaji wake na kusema watu wamekuwa wakipotosha umma.


Dkt. Abbasi amesema kuwa Sheria na 12 ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 kifungu cha 51 kinatoa ruhusa kwa chombo cha habari kukosoa kwa lengo la kuonyesha njia mbadala katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.


“Hakuna chombo cha habari kitakachochukuliwa hatua kwa kukosoa, haki hiyo ipo kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 kifungu cha 51, tutaendelea kuthamini na kufanyia kazi ukosoaji huo,” alisema Dkt. Abbasi.


Mbali na hilo Dkt. Hassan Abbasi amedai kuwa kama serikali haitasita kuvichukulia hatua vyombo vya habari vyote ambavyo vitakiuka sheria na misingi ya maadili ya taaluma ya habari kwa lengo la kulinda maslahi ya taifa. 


Dkt. Abbasi alisitiza kuwa ni vyema wamiliki wa vyombo vya habari wakatumia uhuru huo wa kisheria kuchapisha habari zenye nia njema kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi badala ya kueneza hofu miongoni ya mwa jamii.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search